25.7 C
New York

‘Still Mshua EP’ ya Mau Music yazidi kupenya

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MSANII wa Bongo Fleva anayefanya kazi zake nchini Afrika Kusini, Mau Music, ameendelea kutamba mitandaoni na kwenye majukwaa ya muziki baada ya kuachia albamu yake fupi Still Mshua, ambayo kwa sasa inaonyesha mafanikio makubwa.

Kwa muda mrefu, Mau Music amekuwa miongoni mwa wasanii wanaoutambulisha muziki wa Bongo Fleva nchini Afrika Kusini, akichanganya ladha na lugha za pande zote mbili, hatua iliyompa umaarufu wa kuwa MswaZulu.

Akizungumzia kazi hiyo, Mau Music alisema Still Mshua inajumuisha vibao kadhaa vikiwamo Sawa, Million Monsters, Oyoyo, No One, Lukelu, Champion, Swali na Iqolo.

“EP kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki duniani. Nawashukuru wasanii wakubwa kama Jay Moe, Mr Blue, Music Holiq, Prince Papito, G Funk SA, Dinkii, Kamungu, Papi na Dan Cruz kwa kushiriki kunipa ladha bora zaidi. Naamini hii ndiyo EP bora kwa mwaka huu, namba zake zinanitia moyo na ninaendelea kuisukuma ifike kwa mashabiki wa Afrika na duniani kote,” amesema Mau Music.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img