RIO Brazil
BUNGE la Brazil limewasilisha mswada wa kuomba Rais wa zamani wa Taifa hilo, Jair Bolsonaro, kupunguziwa adhabu ya kifungo cha gerezani.
Bolsonaro mwenye umri wa miaka 70, kwa sasa yuko gerezani akitumikia kifungo cha miaka 27 alichohukumiwa mwezi uliopita.
Mwanasiasa huyo alihukumiwa baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka ya kupanga maandamano ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita wa mwaka 2022.
Hata hivyo, mapema jana bunge hilo lilikumbwa na vurugu uku wabunge wa kihafidhina wakiendelea kushinikiza sheria ambayo ingepunguza adhabu ya kifungo cha rais wa zamani wanchi hiyo Jair Bolsonaro.
Mbunge mmoja wa mrengo wa kushoto aliondolewa kwa nguvu na polisi baada ya kujaribu kuvuruga shughuli, huku video zikionesha hali ya taharuki ikizuka wakati maafisa usalama wakijaribu kurejesha utulivu.
Wakati huo, Bolsonaro alinga kile alichokiita kuwa ni hujuma iliyopelekea kupoteza nafasi ya kurudi madarakani mbele ya aliyekuwa mpinzani wake katika kinyang’anyiro cha urais, Luiz Inacio Lula da Silva.
Endapo muswada huo wa Bunge utapitishwa, huenda mwanasiasa huyo akatimikia chini ya miaka miwili tu kifungo chake cha sasa.
Kwa upande mwingine, wanasheria wa Bolsonaro wamepeleka ombi lao kwa Mahakama Kuu wakitaka mteja wao kuachiwa ili akafanyiwe matibabu.
Ni katika ombi lao hilo, wameshauri aachiwe na kutumikia kifungo chake akiwa nyumbani kutokana na kile walichokiita kuwa ni sababu za kibinadamu.


