LOS ANGELES, Marekani
HATIMAYE staa wa muziki wa Hip hop, Sean Combs ‘P. Diddy’, atatumikia kifungo cha miezi 50 gerezani, sawa na miaka minne na miezi miwili.
Mahakama imemshushia rungu hilo baada ya kumkuta na hatia katika kesi zake za udhalilishaji wa kijinsia zilizokuwa zikimkabili mwanamuziki huyo.
Sambamba na adhabu hiyo, pia P. Diddy ametakiwa kulipa faini ya Dola za Marekani 500,000 (zaidi ya Sh bil. 1.2 za Tanzania).
P. Diddy anakuwa staa wa pili kwa miaka ya hivi karibuni kuingia gerezani kwa mashitaka ya aina hiyo baada ya R. Kelly aliyehukumiwa miaka 31.
Baada ya P. Diddy kuhukumiwa, aliyewahi kuwa mpenzi wake, Cassie Ventura, ambaye pia alimfungulia mashitaka ya unyanyasaji wa kijinsia, aliibua madai kuwa anahofia usalama wake.
“Hofu yangu ni namna familia na watu wa karibu wa P. Diddy watakavyopokea hukumu hii. Nimelazimika kuihamisha familia yangu jijini New York.
“Kwa sasa, naishi maisha ya kujificha kwa kuwa sijui nini kitatokea endapo nitajichanganya kwenye maeneo yenye watu wengi,” amesema Cassie.
Published:


