6.4 C
New York

Staa Marekani jela kwa wizi wa TV

Published:

LOS ANGELES, Marekani
MWANAMUZIKI maarufu nchini Marekani, Sean Kingston, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu na nusu gerezani katika kesi yake ya wizi.
Kingston, pamoja na mama yake mzazi, walikuwa wakituhumiwa kwa wizi wa vitu vyenye thamani, ikiwamo runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 232.
Pia, wawili hao walitajwa kuiba saa na kifaa maalumu cha kuzuia risasi, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Pauni 738,000.
Akiwa mahakamani, Kingston alikiri makosa, akiomba radhi kwa ahadi kuwa asingerudia, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.
Mama yake, Janice Turner, alishahukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani tangu Julai, mwaka huu.
Kwa mashabiki wa muziki, wanafahamu kuwa Kingston aliwahi kuwika kupitia nyimbo ‘Fire Burning’, ‘Take You There’ na ‘Eenie Meenie’ aliomshirikisha Justin Bieber.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img