Na Mwandishi Wetu
Msanii Harmonize leo Mei 19,2025 amefika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Basata, Dk. Kedmon Mapana, kuhusu maendeleo ya sanaa nchini ikiwa ni siku chache baada ya kumalizana na msanii Ibraah.
Hivi karibuni Harmonize alitangaza kumruhusu msanii Ibraah kuondoka katika lebo yake ya Konde Gang bila kulipa chochote baada ya awali kutakiwa kulipa sh 1 bilioni ili kuruhusiwa kufanya kazi zake nje lebo hiyo.

Baada ya kutoka Basata, Harmonize aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika katika baraza hilo kwa sababu ni wajibu wake kufika kuelezea msimamo wake kwa viongozi hao ambao walikuwa na haja ya kujiridhisha.


