28.2 C
New York

Angelina Jolie: Aliishi maisha ya ndoa akiwa na miaka 14

Published:

LOS ANGELES, Marekani

JINA la Angelina Jolie haliwezi kuwa geni masikioni mwa wapenzi wa filamu duniani. Ni mwigizaji na prodyuza maarufu katika soko la Hollywood, akitwaa tuzo kubwa nyingi.

Kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye gemu, haishangazi kuona akitwaa Academy Award, Tony Award na Golden Globe Award aliyobeba mara tatu.

Filamu alizoigiza bibiye huyo aliyezaliwa mwaka 1975 zimeingiza si chini ya Dola bilioni 6.9 duniani kote. Ndiyo maana anatajwa kuwa mwigizaji wa kike ghali zaidi Marekani.

Jolie (51), anatokea katika familia ya waigizaji, ambapo baba, Jon Voight, na mama yake, Marcheline Bertrand, walikuwa mastaa wa filamu.

Voight ni Mwingereza mwenye asili ya Slovakia, wakati Marcheline ni raia wa Uholanzi akiwa na asili ya Canada.

Taarifa rasmi zinathibitisha kuwa Jolie ana undugu na Waziri wa Fedha zamani wa Uholanzi, Wim Kok, ambaye baadaye alikuja kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Akiwa na umri wa miaka 14 tu, tayari Jolie alikuwa na mpenzi na mama yake ndiye aliyewaruhusu kuishi pamoja pale nyumbani.

“Tulikuwa tunaishi chumba kimoja, huku mama akiwa chumba kingine. Niliendelea kwenda shule na mahusiano yangu yakawa salama zaidi,” alisema Jolie.

Alisema kwake mahusiano hayo hayakuwa na tofauti na ndoa hadi yalipovunjika na kuamua kujikita kwenye sanaa ya uigizaji.

Uhusiano wake wa kwanza akiwa mkubwa ni ule wa mwigizaji mwenzake, Jonny Lee Miller, mwaka 1995, ambaye walianzia ‘lokesheni’ wakati wa kurekodi filamu ya ‘Hackers’.

Jolie alianza kuonekana kwenye filamu akiwa mdogo, alipoigiza ‘Lookin’ to Get Out’ akiwa na baba yake, Jon Voight. Hiyo ilikuwa mwaka 1982.

Hata hivyo, filamu yake ya kwanza akiwa mkubwa ni ‘Cyborg 2’ (1993), kisha ikafuata ‘Hackers’ (1995), ‘George Wallace’ (1997) na ‘Gia’ (1998).

Filamu zingine alizowahi kuigiza na kumpa umaarufu mkubwa ni ‘Lara Croft: Tomb Raider’ (2001), ‘Mr. & Mrs. Smith’ (2005), ‘Wanted’ (2008), na ‘Salt’ (2010).

Wakati fulani, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo mwenzake, Jenny Shimizu, ambaye ni mwigizaji na mwanamitindo maarufu nchini Marekani.

Walikutana ‘lokesheni’ mwaka 1996 wakati wa kurekodi filamu ya ‘Foxfire’. “Nilimpenda sekunde chache tu baada ya kumuona.

Kwa mujibu wa Shimizu, uhusiano wao uliendelea kwa siri hata Jolie alipokuwa na wanaume wengine kwa nyakati tofauti.

Baadhi ya wanaume wengine aliowahi kutoka nao Jolie ni Billy Bob Thornton, Timothy Hutton, na Brad Pitt ambaye hata hivyo waliachana rasmi mwaka 2019.

Bibiye huyo ana watoto sita; watatu amewaasili, akiwamo Zahara Marley aliyemchukua Ethiopia akiwa na miezi sita, na watatu ni wake aliowapata akiwa na Pitt.

Kati ya hao watatu, wawili ni mapacha, Knox Leon na Vivienne Marcheline, waliozaliwa mwaka 2008.

Related articles

Recent articles