22 C
New York

Wagonjwa wa ‘AI’ kutumika mafunzo ya udaktari

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

DUNIA inakwenda kasi. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaibua gunduzi zinazorahisha na kuleta ufanisi wa shughuli mbalimbali.

Kwa sasa, fani ya udaktari nayo nchini Uingereza imeanza kunufaika na teknolojia ya akili-mnemba (AI), ambapo ametengenezwa mgonjwa feki atakayetumika kwa mafunzo.

Kama ambavyo huwa kati ya daktari na mgonjwa, ‘binadamu’ huyo aliyetengezwa ana uwezo wa kuzungumza na kueleza hisia zake.

Hiyo inawasaidia wanafunzi wa fani ya udaktari kuzungumza naye, kuchukua maelezo yake juu ya tatizo lake, kisha kujua aina ya tiba anayopaswa kupatiwa.

Ni ‘binadamu’ aliyetengezwa, ambaye wanafunzi wa fani ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Bristol wanamtumia kama mgonjwa wa kufanyia mazoezi.

Dk. Chris Jacobs, ambaye pia ni muhudumu katika Hospitali ya Great Western, anasema: “Kutumia gunduzi za aina hii kunafanya mafunzo kuwa rahisi zaidi kwa wanafunzi, tofauti na kutumia vitabu pekee.

“Nafikiri tunahitaji kuendelea kubuni, tunahitaji kuendelea mifano ya aina hii katika sekta ya afya na kuona matokeo yanayokuja.”

Hatua hii kubwa katika sekta ya afya inatanguliwa na ile ya nchini China, ambapo baadhi ya roboti zimeanza kujaribiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img