LAGOS, Nigeria
WARATIBU wa Shindano la Big Brother Naija wametangaza msimu mpya wa 2026, huku wakitaja zawadi iliyovunja rekodi ya miaka iliyopita.
Kwa msimu huu wa 11, mshindi atajiondokea na kitita cha Naira milioni 160 (zaidi ya Sh Mil. 305 za Tanzania).
Kwa mujibu wa taarifa yao, msimu huu mpya wa 11 wa Shindano hilo unatarajiwa kuanza Julai 26, 2026.
Zawadi hiyo ya Naira milioni 160 ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya Big Brother Naija lililoanza mwaka 2006.
Ifahamike kuwa ushiriki wa Shindano hilo ni bure, ingawa ni kwa wenye umri usiopungua miaka 21.


