WASHINGTON DC, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amedai kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, anajiandaa kujiuzulu.
“Keir Starmer atajiuzulu katika nafasi yake ya Waziri Mkuu wa Uingereza. Amechemsha sana katika mambo nyeti mawili – uhamiaji na nishati,” amesema Rais Trump.
Kauli yake inakuja baada ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kutoa taarifa kama hiyo.
Katika taarifa iliyotolewa na BBC, Waziri Mkuu huyo atajiuzulu Jumatatu ya wiki ijayo (Juni 22, 2026).
Waziri Mkuu, Starmer, anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu hata kutoka katika Chama chake cha Labour.


