32 C
New York

Akon: Wanamuziki wana majina, hawana pesa

Published:

LOS ANGELES, Marekani

SUPASTAA wa muziki raia wa Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon, amesema wasanii wengi wa sanaa hiyo wana majina makubwa lakini hawana kipato kikubwa kama wanavyochukuliwa na jamii.

Akon amesema licha ya maisha ya kifahari wanayoposti mitandaoni, wengi wao wana maisha ya kuungaunga huko mitaani.

Ameongeza kuwa wanaonufaika zaidi na fedha za muziki ni viongozi wanaosimamia kazi za muziki na si wanamuziki.

“Katika soko la muziki, msanii ni mtu wa mwisho kulipwa. Msanii ni maarufu lakini hana maisha. Kama unataka kuwa na jina bila pesa, basi kuwa msanii,” amesema Akon.

Katika hatua nyingine, Akon amewataka wasanii kichungulia fursa zingine nje ya muziki, badala ya kutegemea kuimba tu.

Related articles

Recent articles