Na Christopher Msekena, Gazetini
MSANII wa muziki wa Injili anayeishi Ireland, Sela Mulonda, amewashukuru mashabiki kwa mapokezi makubwa wimbo wake mpya ya Búlamu.
Sela Mulonda mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ameendelea kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki Afrika Mashariki kwa nyimbo za sifa.
Akizungumza na gazetini.com, Sela Mulonda amesema ndani ya muda mfupi tangu kuachiwa kwa wimbo huo, Búlamu imefanikiwa kupata wasikilizaji na watazamaji wengi zaidi ya matarajio yake.
«“Búlamu imenifungulia njia zaidi huko nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Nimepata idadi kubwa ya watazamaji kwenye chaneli yangu ya YouTube, naamini mashabiki wanaendelea kunipa sapoti ili kwa pamoja muziki wetu ufike mbali,” amesema Sela Mulonda.


