18.4 C
New York

Yanga, Simba kama Arsenal, Man City tu hesabu za ubingwa

Published:

Na Hassan Mwasha,Gazetini

KWA mashabiki wa soka wa Tanzania, macho na masikio yao yameelekezwa katika vita mbili kubwa. Ubingwa wa Ligi Kuu Bara na ile ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Kote huko, tofauti ni pointi mbili tu kati ya timu mbili za juu kwenye msimamo, ambapo kwa Ligi Kuu Bara, Yanga iko kileleni ikiwa na pointi 54, huku Simba ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 52.

Kwa England, Arsenal nayo iko kileleni baada ya kukusanya pointi 79, ikifuatiwa na Manchester City yenye 77, huku kila timu ikiwa imeshacheza mechi 36.

Kwamba wakati Yanga na Simba zikiwa zimebakiza mechi saba kila moja, Arsenal na Man City zina mbili tu mkononi kumaliza msimu wa 2025-26.

VIPIGO BONGO, EPL VINAFANANA

Wakati Yanga ikiwa imeshatembeza vipigo 16 katika mechi 23, Simba wao wameshinda mara 15. Ni tofauti ya ushindi wa mechi moja kama ilivyo kwenye vita ya Arsenal na Man City.

Katika mechi 36, Washika Bunduki wameshinda 24, wakati Man City ya Pep Guardiola imetembeza vipigo 23. Tofauti ya ushindi wa mechi moja kama ilivyo Bongo.

Hata kwa upande wa sare iko hivyo; Yanga wana sare saba msimu huu wa Ligi na Simba wana nane. Arsenal wana sare saba, huku City wakiwa na nane.

Pia, wakati Yanga ikiwa imefungwa mechi moja, kama ilivyo kwa Simba, Arsenal na Man City nazo zimefanana kwa kila moja kufungwa mara tano kwenye Ligi.

MECHI ZILIZOBAKI YANGA, SIMBA

Kwa upande wa Yanga, imebakiza mechi dhidi ya Singida Black Stars (nyumbani, Mei 22, 2026), Namungo (nyumbani, Mei 25, 2026), Mashujaa (ugenini, Juni 13, 2026), Fountain Gate (ugenini, Juni 17, 2026), Azam (nyumbani, Juni 24, 2026), TRA (nyumbani, Juni 27, 2026), na JKT (ugenini, Juni 30, 2026).

Simba wao watacheza dhidi ya Coastal Union (ugenini, Mei 21, 2026), Dodoma Jiji (nyumbani, Mei 24, 2026), Pamba Jiji (nyumbani, Juni 14, 2026), Mbeya City (ugenini, Juni 18, 2026), Mtibwa Sugar (Juni 24, 2026), Singida Black Stars (nyumbani, Juni 27, 2026), na KMC (nyumbani, Juni 30, 2026).

ARSENAL, YANGA UGENINI, CITY NA SIMBA UGENINI

Arsenal watacheza na Burnley (Mei 18, 2026), kabla ya kufunga dimba na Crystal Palace (Mei 24, 2026). Man City wao wana mechi dhidi ya Bournemouth (Mei 19, 2026) na Aston Villa (Mei 24, 2026).

Kwamba Yanga, kama ilivyo kwa Arsenal, itamalizia ugenini, wakati Simba na Man City zitafunga msimu zikiwa nyumbani, ingawa Ligi Kuu ya England itatangulia wiki moja kumalizika, kabla ya hii ya Tanzania.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img