22.9 C
New York

Mwanaume anayetaka nipike hanifai

Published:

LAGOS, Nigeria

ALIYEWAHI kuwa mshindi wa Shindano la Big Brother Naija, Mercy Eke, amezua mjadala mzito mitandaoni kwa kauli yake ya kusema hawezi kuolewa na mwanaume anayetaka awe anapika.

Si tu kuolewa, bali pia Mercy amesema hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume anayetaka afanye hivyo.

Kwa mujibu wake, anaweza kupika pale anapojisikia, na si kufanya mara kwa mara ndani ya nyumba.

“Siwezi kuolewa au kuwa na mpenzi anayetaka niwe nampikia. Napika mara moja tu ninapojisikia. Kama unataka kupikiwa, ajiri mpishi,” amesema.

Kauli yake hiyo imezua gumzo kutoka kwa mashabiki wake mitandaoni, wengine wakisema bibiye huyo hajitambui.

Related articles

Recent articles