22.9 C
New York

Mbappe mfungaji bora, aweka rekodi

Published:

MIAMI, Marekani

STRAIKA wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Kyian Mbappe, ndiye aliyeibua na tuzo ya Mfungaji Bora wa msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia (2026).

Licha ya Ufaransa kuishia nusu fainali, Mbappe amebeba tuzo hiyo baada ya kumaliza akiwa na mabao 10 katika mechi nane alizocheza.

Nyota huyo wa Real Madrid anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya michuano hiyo kutwaa mara mbili tuzo ya Mfungaji Bora.

Wakati huo huo, anakuwa mchezaji wa pili baada ya mkongwe Gerd Muller kufikisha mabao 10 ndani ya msimu mmoja wa Kombe la Dunia.

Pia, Mbappe anakuwa mfungaji bora wa muda wote wa fainali za Kombe la Dunia baada ya kufikisha mabao 22, akimzidi bao moja Lionel Messi.

Related articles

Recent articles