26.5 C
New York

Barca yanasa winga Ubelgiji

Published:

CATALUNYA, Hispania

KLABU ya Barcelona imekamilisha usajili wa winga kutoka Club Brugge ya Ligi Kuu nchini Ubelgiji, Jesse Bisiwu.

Aliyefichua kukamilika kwa dili hilo ni mwandishi wa habari maarufu wa Italia, Fabrizio Romano.

Romano anayesifika kwa taarifa zake za usajili, amedai kuwa Barcelona imemsajili kwa ada ya euro milioni 8.

Katika mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 kuna kipengele kinachoihakikishia Club Brugge asilimia 20 ya fedha za usajili endapo atauzwa na Barcelona.

Usajili wake ni sehemu ya mikakati ya kocha wa Barcelona, Hansi Flick, kujiandaa na msimu ujao (2026-27) wa La Liga na michuano mingine.

Related articles

Recent articles