26.5 C
New York

Aliyefariki mikononi mwa polisi aibua maandamano

Published:

MILAN, Italia

MAELFU ya raia wa Italia wameingia barabarani kulaani taarifa za kifo cha mwenzao aliyefariki akiwa anashikiliwa na polisi huko Kaskazini mwa Mji wa Bologna.

Maadamano hayo ni ya kushinikiza uchunguzi wa haki juu ya kifo cha mzaliwa huyo wa Morocco aliyefahamika kwa jina la Abderrahim Fakir.

Moja ya video zilizosambaa mitandaoni imewaonesha polisi wawili wakiwa wamemlaza kifudifudi, huku wakiwa wamemkalia mgongoni.

Katika tukio moja, waandamanaji wameonekana wakipigana na polisi. Waendesha mashitaka wamedai kuwa polisi 64 wamejeruhiwa katika vurugu hizo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, amekiri kuwa uchunguzi unahitajika, ingawa ameeleza kuwa hakubaliani na vurugu hizo.

Related articles

Recent articles