11.6 C
New York

Tunachofahamu kuhusu matumizi ya gesi asilia Tanzania

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

KWA mujibu wa Serikali hadi Aprili 2026 jumla ya nyumba 2,512 zimeunganishwa na huduma ya gesi asilia katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza matumizi ya nishati safi nchini.

Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na nyumba 880 zilizounganishwa, ukifuatiwa na Lindi nyumba 677, Pwani nyumba 530 na Mtwara nyumba 425.

Amesema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania inaendelea kutekeleza miradi ya kusambaza gesi asilia ili kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo kwa wananchi wa mijini na vijijini.

Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini inaendelea kusambaza mitungi 452,445 ya gesi ya LPG yenye ujazo wa kilo sita kwa ruzuku ya asilimia 50 ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika maeneo ya vijijini na vijiji-miji.

Serikali pia imeeleza kuwa inaendelea kufanya tafiti kubaini miundombinu bora ya usambazaji wa gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza kwenye usambazaji wa gesi hiyo ili wananchi wengi zaidi wanufaike na nishati safi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img