11.2 C
New York

Heavenly Voice Gospel Band kuwafikia mashabiki

Published:

Na Mwandishi Wetu

Heavenly Voice Gospel ambayo ni bendi ya muziki wa injili yenye maskani yake Marekani, imesema imeandaa nyimbo nyingi za kuwabariki mashabiki duniani kote.

Akizungumza na tovuti hii, msemaji wa Heavenly Voice Gospel Band, Brazzoff Mwibelecha, amesema tayari wana nyimbo nyingi na wanajiandaa kufanya live recoding hivyo mashabiki wakae tayari.

“Kundi hili la sauti ya mbinguni ina mambo mengi sana, kwa msaada ya Mungu tumejiandaa vya kutosha kwa nyimbo nyingi zenye upako, muhimu ni sapoti yako maana bila hivyo hatuwezi kufika mbali,” amesema Brazzoff.

Aliongeza kwa kutaja baadhi ya waimbaji wachache kwenye bendi hiyo kuwa ni Rachel Saleh ambaye ni kiongozi wa nidhamu, Mao Kakozi ambaye ni kiongozi wa muziki (Music Director), Vyizigiro Emelina, Tuyishime Sifa, na Christina Niyo wakiwa ya chini ya Mchungaji Kiongozi Dk Vitalis Kyulule.

Naye mwanzilishi na mwalimu wa bendi hiyo, Maisha Manase, amesema Mungu alimpa maono ya kuanzisha Heavenly Voice Gospel Band na ameanza mipango yake na kuwahudumia mashabiki wao.

“Kuna msemo unaosema ‘follow you’re dream’ nilifatisha ndoto zangu, niliona nikiunganisha timu kama hivi kwa pamoja wengi wanaweza kubarikiwa na sasa tumeanza kukimbiza ndoto zetu za kumtumikia Mungu japo kuwa changamoto ni nyingi hasa za kifedha pale tunapoalikwa kwenye huduma mbali na nyumbani, hivyo tunamuomba Mungu atuinulie watu watakaotubeba kwenye hilo,” anasema Maisha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img