13.5 C
New York

Minaj kuibukia sherehe ya waandishi wa Ikulu

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

KIPENZI cha Rais Donald Trump, Nicki Minaj ni miongoni mwa mastaa wa muziki watakaohudhuria halfa ya chakula cha jioni itakayofanyika kesho Aprili 26, 2026.

Hafla hiyo ya kila mwaka ni ya Chama cha Waandishi wa Habari wanaoripoti habari za Ikulu na Rais Trump.

Minaj amekuwa rafiki mkubwa wa Rais Trump, ambaye hii itakuwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria hafla hiyo akiwa kiongozi wa nchi.

Katika awamu yake ya kwanza madarakani, alikataa mwaliko, kama ambavyo pia alifanya mwaka jana.

Supastaa mwingine wa muziki, Nelly, ameripotiwa kuwa atapanda jukwaani kutumbuiza katika hafla hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img