6.4 C
New York

Miji inayoongoza kwa mishahara minono duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

UTAFITI wa Deutsche Bank umefuatilia maisha ya miji 69 duniani na kubaini tofauti iliyopo katika mishahara wanayolipwa wafanyakazi kila mwezi. Aidha, ajira zinazozalisha mishahara mikubwa hiyo ni pamoja sekta ya fedha na teknolojia.

Sasa, kwa mwaka huu, 2025, mji unaoongoza kwa mishahara mikubwa ni Geneva, Uswis, ambapo mfanyakazi analipwa wastani wa Dola za Marekani 7,984 Kwa mwezi.

Katika utafiti huo, Mji wa Zurich, ambao pia uko Uswis, unashika nafasi ya pili ukiwa na wastani wa mshahara wa Dola 7,788.

San Francisco wa Marekani unashika nafasi ya tatu, utafiti ukieleza kuwa wastani wa mshahara wa mwezi ni Dola 7,092, ukiwa ndiyo Mji unaolipa vizuri zaidi wafanyakazi nchini humo.

Miji mingine ambayo wafanyakazi wanafurahia mishahara mikubwa zaidi ni Luxembourg (Dola 6,156), Boston (Dola 5,940), Chicago (Dola 5,203) na New York (Dola 5,128).

Kwa upande mwingine, miji inayotajwa na utafiti kuwa na mishahara midogo ya kila mwezi ni pamoja na Cairo (Dola 165), Bogota (Dola 375) na Rio de Janeiro (Dola 439).

Pia, licha ya Japan kupiga hatua kubwa ya kiuchumi duniani, hasa kutokana na maendeleo ya teknolojia, Mji Mkuu wake, Tokyo, haupo kwenye orodha ya miji 10 inayoongoza kwa mishahara minono duniani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img