5.7 C
New York

Dhana potofu juu ya saratani ya mapafu

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SARATANI ya mapafu ni miongoni mwa magonjwa tishio ulimwenguni, ukitajwa kusababisha vifo zaidi ya milioni 1.8 kwa mwaka.

Takwimu hizo ni za mwaka 2020, hivyo huenda idadi ya vifo imeongezeka zaidi kwa kipindi cha miaka mitano ya hivi karibuni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kansa ya Tisch ya mjini New York, Dk. Fred R. Hirsch, anasema licha ya hatari kubwa inayosabishwa na saratani ya mapafu, bado kumekuwapo na taarifa za upotoshaji juu ya ugonjwa huo.

Mosi, si kweli kwamba uvutaji wa sigara ndiyo chanzo pekee cha ugonjwa wa saratani ya mapafu. “Si kweli. Na hii kwa bahati mbaya imekuwa ikipotosha wengi,” anasema Dk. Hirsch.

Kwa Marekani, asilimia 10 hadi 20 ya wagonjwa wa saratani ya mapafu hawajawahi kuvuta sigara. Kwa wengine, hawajafikisha hata sigara 100 katika maisha yao,” anasema.

Kwa mujibu wake, saratani ya mapafu pia huweza kusababishwa na historia ya familia, hewa chafu, mionzi na hata magonjwa sugu ya mapafu.

Hata hivyo, Dk. Tisch anasisitiza kuwa mtu anayekuwa karibu na mvutaji wa sigara na kufikiwa na moshi, naye anakuwa hatarini kupata ugonjwa huo.

“Wasiovuta sigara lakini wakawa wanafikiwa na moshi wakiwa nyumbani au kazini, wana asilimia 20 hadi 30 ya kupata saratani ya mapafu,” anasema.

Pili, ipo dhana potofu kuwa saratani ya mapafu ni ugonjwa wa wazee. Ni kutokana na takwimu zinazoonesha kuwa wengi kati ya wagonjwa wana umri wa miaka zaidi ya 65.

“Si kweli. Kwa sasa, kuna vijana wengi wenye umri chini ya miaka 50, hasa wanawake, na tayari wana ugonjwa wa saratani ya mapafu,” anasema Dk. Tisch.

Tatu, ni dhana potofu kwamba upasuaji wa saratani ya mapafu husababisha ugonjwa huo kuenea zaidi. “Hapana. (upasuaji) hauifanyi saratani kuenea,” anasema Dk. Tisch.

Aidha, anasisitiza kuwa upasuaji wa saratani ya mapafu unapaswa kufanywa katika hatua za mwanzo za ugonjwa. “Katika hatua hii, mgonjwa anaweza kupona kabisa,” anasema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img