9.3 C
New York

Usichokijua mazungumzo ya Rais Trump, Mfalme wa Saudi Arabia

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
KWA mara ya kwanza tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Palestina katika Ukanda wa Gaza, Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, amekutana na Rais Donald Trump mjini Washington.
Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo leo Novemba 18, huku wachambuzi wa siasa wakiuita kuwa ni Mkutano wa kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya mataifa mawili hayo.
Kwa mujibu wa wachambuzi, Mkutano kati ya Bin Salman na Rais Trump ulitarajiwa kujadili masuala mbalimbali, ikiwamo ulinzi, teknolojia na pia utaigusia Israel.
Ziara ya mwisho ya Bin Salman nchini Marekani ilikuwa mwaka 2018, ambayo hata hivyo iligubikwa na kashfa ya Serikali yake kumuua mwandishi wa habari wa nchi hiyo, Jamal Khashoggi.
Tangu na hata kabla ya hapo, Marekani na Saudi Arabia zimekuwa na uhusiano mzuri na hata Rais Trump aliporejea madarakani Januari, mwaka huu, ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi ilikuwa ni kuitembelea Saudi Arabia.
Akiwa mjini Riyadh, Rais Trump aliutangazia ulimwengu kuwa Saudi Arabia ina uwekezaji wa Dola milioni 600 nchini Marekani.
Safari, miongoni mwa maeneo mengine yaliyotarajiwa kuwa ajenda ya Mkutano wa Rais Trump na Bin Salman ni uwekezaji, masuala ya nyuklia na akili-mnemba (AI).
Masuala ya usalama katika eneo la Mashariki ya Kati ni ajenda nyingine muhimu, hasa kutokana na kile kilichotokea Juni, mwaka huu, ambapo Israel na Marekani zilishambulia vinu vya nyuklia nchini Iran.
Wachambuzi wanaamini Saudi Arabia inatamani kuhakikishiwa usalama, kama ambayo Marekani imefanya kwa Qatar baada ya kushambuliwa na Israel katika tukio la Septemba, mwaka huu.
Ikumbukwe, Saudi Arabia haikubaliani na Israel juu ya mgogoro wake na Palestina. Serikali ya Bin Salman inataka kuona Israel ikipewa uhuru na kutambulika kama nchi inayojitawala.
Hivyo, kupitia Mkutano wa leo, Saudi Arabia ilitarajiwa kuishawishi Marekani iunge mkono jitihada za Palestina kujitafuta kama Taifa huru.
Katika hatua nyingine, iliaminika kuwa Rais Trump angetumia Mkutano wake na Bin Salman kuiomba Saudi Arabia iunge mkono jitihada zake za kurejesha utulivu katika Ukanda wa Gaza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img