28.1 C
New York

Mambo ni moto msimu mpya Ligi Kuu za Ulaya: Bundesliga

Published:

MUNICH, Ujerumani

BAYERN Munich itakuwa nyumbani kuikaribisha VfB Stuttgart katika mechi ya ufunguzi wa Bundesliga msimu mpya wa 2026-27. Hiyo itakuwa Ijumaa ya Agosti 28, 2026.

Je, nani kumfunika Harry Kane, ambaye msimu uliopita aliibeba kiatu cha ufungaji bora akiwa ameingia kambani mara 36?

Bayern chini ya kocha Vincent Kompany, ilimaliza msimu ikiwa na mataji mawili, ingawa haikuweza kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kane (33), ameshafunga mabao 98 katika mechi 94 za Bundesliga alizocheza tangu asajiliwe na Bayern akitokea Tottenham.

Mbaya kwa wapinzani, Kane amekuwa akishirikiana na Michael Olise na Luis Diaz kuifanya safu ya ushambuliaji ya Bayern kuwa ya moto kweli kweli.

Kama hiyo haitoshi, mabosi wa Bayern wameingia sokoni majira haya ya kiangazi na kuongeza mshambuliaji raia wa Morocco, Ismael Saibari.

Upinzani katika mbio za ubingwa unazihusisha pia Borussia Dortmund, RB Leipzig na Bayer Leverkusen.

Wakati huo huo, Schalke 04 wamerejea vitani baada ya miaka mitatu ya kukosekana Ligi Kuu. Mechi yao dhidi ya Dortmund ni moja ya ‘derby’ zinazosubiriwa.

Elversberg, licha ya kutokea katika Mji wa Spiesen-Elversberg wenye wakazi 13,000, nayo imetua Bundesliga na mtihani ulio mbele yao ni kuhakikisha hawashuki daraja na kurudi ‘mchangani’.

Related articles

Recent articles