PARIS, Ufaransa
MECHI ya kwanza ya Ligi Kuu hiyo ya Ufaransa kwa msimu wa 2026-27 itachezwa Ijumaa ya Agosti 21, 2026. Marseille watakuwa nyumbani kuivaa Strasbourg.
PSG ni mabingwa watetezi wakiwa wamelitwaa taji hilo kwa misimu mitano mfululizo. Wamelikosa mara mbili tu katika misimu 15 ya hivi karibuni.
Msimu uliopita, walifungwa mechi sita pekee, pia wakibeba kwa mara ya pili mfululizo taji la Liga ya Mabingwa Ulaya walioifunga Arsenal katika mechi ya fainali.
Kikosi chao kimeimarishwa kwa usajili wa kiungo kutoka Monaco, Maghnes Akliouche, na beki wa kushoto aliyetokea Aston Villa, Lucas Digne.
Aidha, Monaco, mabingwa wa msimu wa 2016-17, na Lille (2020-21), wanatarajiwa kuipa upinzani PSG katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu.
Wababe wa zamani, Marseille, wanaopitia hali mbaya ya kiuchumi, hivyo hawaja bize sokoni, na mbaya zaidi wamempoteza mshambuliaji wao, Mason Greenwood, ambaye ametimkia Uturuki.
Kwa upande wa makocha, Will Still ametua Auxerre, wakati Liam Rosenior aliyekuwa Chelsea amejiunga na Paris FC. Beki wa zamani wa Chelsea, Felipe Luis, amepewa mikoba ya kuinoa Monaco.
Lens waliokuwa washindani wakubwa wa PSG msimu uliopita, wako na kocha mpya, Dino Toppmoller, wakati Lille iliyoshika nafasi ya tatu msimu uliopita iko chini ya mtoto wa Carlo Ancelotti, Davide.
Strasbourg nayo ina kocha mpya, Hugo Oliveira, ambaye amechukua nafasi ya Gary O’Neil aliyetimkia Ligi Kuu ya England (EPL).


