LONDON, Uingereza
ARSENAL na Manchester City zitakwana kesho Agosti 16, 2026, mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa katika Uwanja wa Principality mjini Cardiff, Wales.
Ni mchezo utakaokutanisha bingwa wa Ligi Kuu ya England (Arsenal) na yule wa FA (Man City), ukiashiria kufunguliwa kwa pazia la msimu mpya wa 2026-27.
Kocha mpya wa Man City, Enzo Maresca, ataiongoza Man City kwa mara ya kwanza katika mechi ya ushindani tangu alipoajiriwa kurithi mikoba ya Pep Guardiola.
Katika msimu wake wa mwisho, Guardiola aliipa Man City mataji mawili (FA na Kombe la Ligi), huku timu hiyo ikishika nafasi ya pili kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.
Rekodi
Mara ya mwisho kwa Man City na Arsenal kukutana ilikuwa Aprili, 2026, ambapo Guardiola alimtuliza Mikel Arteta kwa kichapo cha mabao 2-1.
Ni mchezo ambao uliochezwa Etihad na mabao ya Man City yalifungwa na Rayan Cherki na Erling Haaland, wakati lile la Washika Bunduki lilipachikwa na Kai Havertz.
Kwa takwimu za jumla, hii itakuwa mechi ya 217 kwa timu hizo kongwe za England kukutana. Arsenal wameshindwa 100 na Man City wamepata ushindi mara 67.
Vikosi
Arsenal – Raya, White, Mosquera, Gabriel, Hincapie, Guimaraes, Lewis-Skelly, Madueke, Odegaard, Tzolis, na Havertz.
Man City – Donnarumma, Nunes, Dias, Gvardiol, Ait-Nouri, Kovacic, Gonzalez, Savinho, Foden, Semenyo, na Marmoush.


