TEHRAN, Iran
HATIMAYE Serikali ya Iran imeibuka na ujumbe wa kusisitiza kuwa bado ndiyo inayodhibiti safari zote za meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
Kuibuka kwa Iran kumetokana na kile alichotangulia kusema Rais Donald Trump, kwamba Marekani inakabiria kuidhibiti njia kuu hiyo ya maji.
Akijibu madai hayo ya Trump, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran, Kazem Gharibabadi, amesema wataendelea kudhibiti Hormuz hadi pale Marekani itakaposalimu amri.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran, Abbas Araghchi, amesema Marekani ndiyo iliyokiuka makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa wiki chache zilizopita.
Katika taarifa nyingine, watu takribani 11 wamepoteza maisha katika shambulizi la Israel huko Kusini mwa Lebanon, kwa mujibu wa Rais wa nchi hiyo ya Mashariki ya Kati, Joseph Aoun.


