13.9 C
New York

Taliban yaachia tena raia wa Marekani

Published:

KABUL, Afghanistan
HATIMAYE Serikali ya Taliban nchini Afghanistan imetangaza kumwachia huru raia wa Marekani aliyekuwa ameshikiliwa kwa miezi tisa.
Januari, mwaka huu, raia wawili wa Marekani waliachiwa baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa kati ya Marekani na Taliban.
Aida, hatua ya kumwachia Amir Amiry ni matokeo ya mazungumzo yaliyosimamiwa na Qatar, kwa mujibu wa taarifa ya Taliban.
Ikumbukwe, Amiry anakuwa raia wa tano wa Marekani kuachiwa na Taliban tangu mwaka huu uanze na alitarajiwa kurudi kwao jana.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Marekani, Marco Rubio, ameishukuru Qatar kwa jitihada zake za kidiplomasia zilizowezesha kuachiwa kwa Amiry.
Hata hivyo, Rubio amesisitiza kuwa bado uongozi wa Dold Trump unapambana kuwarejesha Wamarekani wengi wanaoendelea kushikiliwa Afghanistan.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img