RIO, Brazil
SERIKALI ya Brazil imewanyima vibali vya kuingia nchini humo viongozi wawili waandamizi wa Serikali ya Rais Donald Trump.
Viongozi hao waliomba viza ya kuingia katika nchi hiyo ya Kusini mwa Amerika ili kufuatilia Uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 4, 2026.
Waliokuwa wameomba viza ya kuingia Brazil ni Naibu Katibu Mkuu wa Idara ya Demokrasia, Haki za Binadamu na Ajira, Riley M. Barnes, na msaidizi wake, Samuel Samson.
Katika ziara yao, vigogo hao walipanga kwenda Brazil kukutana na mamlaka za Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa miezi mitatu ijayo.
Taarifa zinaeleza kuwa hatua ya Brazil kuwanyima viza imelenga kuzuia mpango wa Marekani kuingilia mifumo yake ya kidemokrasia.


