6.4 C
New York

Harmonize ajisalimisha Basata

Published:

Na Mwandishi Wetu

Msanii  Harmonize  leo Mei 19,2025 amefika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Basata, Dk. Kedmon Mapana,  kuhusu maendeleo ya sanaa nchini ikiwa ni siku chache baada ya kumalizana na msanii Ibraah.

Hivi karibuni Harmonize alitangaza kumruhusu msanii  Ibraah kuondoka katika lebo yake ya Konde Gang bila kulipa chochote baada ya awali kutakiwa  kulipa sh 1 bilioni  ili kuruhusiwa kufanya kazi zake nje lebo hiyo.

Baada ya kutoka Basata, Harmonize  aliwaambia waandishi wa habari kuwa  amefika katika baraza hilo kwa sababu ni wajibu wake kufika kuelezea msimamo wake kwa viongozi hao ambao walikuwa na haja ya kujiridhisha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img