2.8 C
New York

Kocha Tottenham alia na VAR

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Tottenham, Thomas Frank, amesema lilikuwa ni kosa kubwa kwa teknolojia ya VAR kuwapa penalti wapinzani wao, Newcastle United, katika mchezo wa Jumatatu. Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya England (EPL), Newcastle wakiwa nyumbani walipata penalti ya dakika ya 86 iliyowapa bao la kusawazisha.

Hata hivyo, beki wa Tottenham, Cristian Romero, alifunga bao la ‘dakika za jioni’ na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Kuhusu penalti hiyo, mwamuzi wa kati, Thomas Bramall, alitumia VAR na kujiridhisha kuwa Rodrigo Bentancur alimshika na kumwangusha kwenye boksi beki wa Newcastle, Dan Burn.

Akizungumza baada ya dakika 90 za mchezo, Frank alisema: “Lilikuwa ni kosa la wazi la VAR. Kwa upande wangu, ile haikuwa penalti.”

Hata hivyo, haikuwa kwa kocha huyo pekee, bali hata baadhi ya wachambuzi wa EPL walikosoa uamuzi huo wa VAR kuipa penalti Newcastle.

Lakini, kwa upande wake, kocha wa Newcastle, Eddie Howe, alisema hakuona tukio hilo uwanjani lakini alirudia kutazama baada ya mchezo kumalizika na kujiridhisha kuwa ilikuwa ni penalti.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img