6.4 C
New York

Mwili wa Joshua warejeshwa nyumbani baada ya kusubiri kwa miaka miwli

Published:

Mwandishi Wetu, Gazetini

BAADA ya miaka miwili ya kusubiri kwa maumivu na wasiwasi, hatimaye mabaki ya mwili wa kijana Mtanzania Joshua Mollel (21) aliyedaiwa kuuawa katika mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 nchini Israel, yamewasili nchini na kukabidhiwa kwa familia yake leo Novemba 19, 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Badala ya tukio la kawaida la mapokezi, leo kulijaa hisia nzito. Wakati viongozi wa Serikali, ndugu na marafiki wakipokea mabaki ya mwili huo, baba yake, Loitu Mollel, alisimama kutoa sauti iliyotetemeka sauti ya mzazi aliyeteseka kimya kimya kwa miaka miwili.

Joshua alikuwa miongoni mwa vijana 260 Watanzania waliokwenda Israel kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kabla ya kutekwa na kuuawa katika uvamizi wa wapiganaji wa Hamas, ambapo pia Mtanzania mwingine, Clemence Mtenga, aliuawa. “Miaka miwili sikuweza kulala,” amesema Mzee Mollel.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mzee Mollel alisema maumivu ya kutopata mwili wa mwanaye kwa muda mrefu yalimuumiza kuliko hata taarifa za kifo chenyewe.

“Miaka yote miwili sikuwa na amani, sikuweza kupata usingizi. Lakini leo namshukuru Mungu… mwili wa mwanangu umepatikana,” alisema kwa uchungu.

Ameishukuru Serikali za Israel na Tanzania kwa ushirikiano uliowezesha kutambulika kwa mabaki hayo kupitia vipimo vya DNA. Serikali: Safari ya mwisho ya Joshua itafanyika kwa heshima

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Said Shaib Musa, amesema Serikali imefuatilia suala hilo tangu siku ya tukio, kupitia Ubalozi wa Tanzania mjini Tel Aviv.

“Tulithibitishiwa Novemba 6, 2025 kuwa mabaki hayo ni ya Joshua. Serikali itaendelea kushirikiana na familia hadi mazishi,” amesema.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho, Novemba 20, katika mtaa wa Njiro, Orkesumet, Simanjiro mahali familia inatarajia kumpumzisha kijana wao ambaye safari yake ya uhai ilikatishwa ghafla na vita vya mbali.

Ujumbe wa amani kutoka Simanjiro

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandana, amesema tukio hilo linaonesha thamani ya amani ambayo Watanzania wanapaswa kuilinda kwa gharama yoyote. “Mapigano haya ndiyo yameondoa kijana wetu. Tuilinde amani yetu,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img