LONDON, Uingereza
MKONGWE wa soka, Zlatan Ibrahimovic, amemtaka Zinedine Zidane kutua katika benchi la ufundi la timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa endapo atarudi kazini.
Ibrahimovic amekuja na ushauri huo kuelekea mechi ya mshindi wa tatu ya msimu huu wa Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na England itakayochezwa kesho (Julai 18, 2026).
Kwa wiki za hivi karibuni, zimekuwapo ripoti nyingi zinazomuhusisha ‘Zizou’ na kibarua cha kuinoa Ufaransa baada ya kocha wa sasa, Didier Deschamps, kusema hatoendelea.
“Zidane alifanya kazi nzuri akiwa kocha wa Real Madrid. Alitwaa mara tatu ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Tunajua anakwenda kuinoa Ufaransa. Najua ataendeleza pale alipoishia Deschamps,” amesema Ibrahimovic.


