25.2 C
New York

Ibrahimovic aanika kilichoiua England kwa Argentina

Published:

MIAMI, Marekani

LEJENDARI wa soka, Zlatan Ibrahimovic, ameibuka baada ya timu ya soka ya Taifa ya England kufungwa mabao 2-1 na Argentina katika mchezo wa usiku wa jana Julai 15, 2026.

Matokeo hayo ya nusu fainali ya Kombe la Dunia yameitoa England na kuipa Argentina tiketi ya kuingia fainali, ambapo itakutana na Hispania (Julai 19, 2026).

Kwa upande wake, Ibrahimovic ameelekeza lawama zake kwa Thomas Tuchel, akisema kocha huyo hakuwa sahihi kutumia mfumo wa kujilinda.

Mkongwe huyo ameeleza kushangazwa na uamuzi wa Tuchel kukimbilia kujilinda na mabeki watano baada ya kupata bao la kuongoza.

Hata kocha huyo raia wa Ujerumani alipoamua kuwaingiza Marcus Rashford na Ivan Toney, mambo yalishakuwa magumu kwa upande wao.

“Alipaswa kumuingiza Rashford mapema ili kushambulia kwa kushitukiza lakini aliamua kujilinda baada ya kufunga bao,” amesema Ibrahimovic.

Related articles

Recent articles