28.2 C
New York

England ya makocha 15 ‘haijatoboa’ Kombe la Dunia

Published:

MIAMI, Marekani 

LICHA ya matumaini makubwa waliyokuwa nayo, mashabiki wa timu ya soka ya Taifa ya England wamelikosa tena taji la fainali za Kombe la Dunia.

Ni miaka 60 imepita tangu walipotwaa ubingwa wa fainali hizo mwaka 1966 na msimu huu safari yao imeishia nusu fainali baada ya kufungwa mabao 2-1 na Argentina ya Lionel Messi.

WACHEZAJI WAPYA 454 

Tangu ilipobeba ‘ndoo’ kwa kuifunga Ujerumani Magharibi mabao 4-2 mwaka 1966, timu ya Taifa ya England imetumia wachezaji wapya 454. 

Nyota mpya wa hivi karibuni katika kikosi hicho ni kinda wa Liverpool, Rio Ngumoha, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza Juni, 2026.

MAKOCHA 15

Tangu Alf Ramsey alipotwaa ubingwa mwaka 1966, makocha wengi wamekalia benchi la ufundi la England lakini hakuna aliyeweza kufikia mafanikio yake hayo. 

Ron Greenwood na Bobby Robson walifeli, kama ilivyokuwa kwa Glenn Hoddle, Sven-Goran Eriksson, Fabio Capello, Gareth Southgate na Tuchel.

MANAHODHA 17

Kwa nyakati tofauti tangu ubingwa wa mwaka 1966, kikosi cha England kimekuwa na manahodha 17, lakini hakuna aliyenyanyua Kombe la Dunia.

Miongoni mwa manahodha hao ni Mick Mills, Bryan Robson, Alan Shearer, David Beckham, Steven Gerrard na Harry Kane.

BADO KIDOGO TU

Tangu mwaka 1966, imetokea mara 12 kwa timu ya Taifa ya England kukaribia kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia.

Miongoni mwanzo ni kuishia hatua ya nusu fainali mara tatu (1990, 2018 na 2026). 

Ni mara mbili tu katika karne hii ya 21 imetokea kwa timu kupoteza nusu fainali ikiwa imetangulia kufunga bao.

Mbaya zaidi, mara zote hizo imeikuta timu ya Taifa ya England – dhidi ya Croatia (2018) na Argentina (2026).

Related articles

Recent articles