10.7 C
New York

Magonjwa yanayoua zaidi Ulaya

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
UTAFITI wa magonjwa ya moyo na kupooza ni chanzo cha vifo vingi zaidi katika nchi za Umoja wa Ulaya (EU), kwa mujibu wa utafiti wa Eurostat.
Ripoti ya utafiti huo iliyotoka Machi, mwaka huu, inaonesha kuwa magonjwa hayo ni chanzo cha vifo milioni 1.7 kwa mwaka 2022 pekee. Ni asilimia 33 ya vifo vyote barani Ulaya.
Utafiti unaeleza zaidi, wengi kati ya waliopoteza maisha kutokana na magonjwa ya moyo ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65.
Pia, ugonjwa wa saratani, ikiwamo ya mapafu, nao ulikuwa tishio kwa mwaka huo, ambapo ulisababisha vifo milioni 1.2, sawa na asilimia 23.
Aidha, utafiti unafichua kuwa saratani ya mapafu ni tishio zaidi kwa wanaume, wakati saratani ya matiti ikiwatesa zaidi wanawake.
Wakati huo huo, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, kama ilivyo Pneumonia, yalikuwa chanzo cha vifo zaidi ya 364,000.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img