6.4 C
New York

Kwanini paka weusi huhusishwa na imani za kishirikina?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
UKIWA kwenye mizunguko yako, hasa nyakati za usiku, ghafla anakatiza paka mweusi mbele yako. Bila shaka, utaanza kuhisi hatari inayohusiana na imani za kishirikina.
Sasa, si tu Tanzania au Afrika, paka wenye rangi hiyo wamekuwa wakihusishwa na ushiriki katika maeneo mengi duniani na hisia hizo hazikuanza leo, jana wala juzi.
Tangu karne ya 18, wachawi walihusishwa kujibadilisha na kutumia mwonekano wa paka mweusi wanapokuwa kwenye ‘kazi’ zao.
Katika mataifa ya Ufaransa na Ubelgiji wakati huo, yalikuwepo matukio ya jamii kuwakamata wachawi na kuwachoma moto wakiwa na paka wao weusi.
Hata hivyo, wakati paka weusi wakionekana ni alama ya ushirikina katika maeneo mengi duniani, hali ilikuwa tofauti nchini Uingereza na Jamhuri ya Ireland.
Katika nchi hizo, endapo ungekutana na paka mweusi ghafla ukiwa njiani au mlangoni kuingia nyumbani kwako, basi ingekuwa ni ishara ya jambo zuri litakalokujia.
Kwa jamii za nchini Scotland, paka mweusi kuingia nyumbani kwako ulikuwa ni ujumbe kuwa utapata bahati, ikiwamo kuingiza fedha bila kutarajia.
Kwa Japan, paka mweusi haikuwa tu ni alama ya bahati na utajiri, bali pia ni kinga dhidi ya magonjwa. Pia, kuwa na paka mweusi kulitajwa kumsaidia mwanamke kuwa na mvuto kwa wanaume.
Kwa upande mwingine, katika karne ya 18, paka weusi walitumiwa na mabaharia, wakiaminika kuwa ni kinga dhidi ya madhoruba wakati wa safari za baharini.
Barani Afrika, wakati huo wa karne ya 18 nchini Misri, paka weusi walitajwa kuwa ni kinga dhidi ya magonjwa kwa wanawake wajawazito na watoto.
Kuhitimisha makala haya, zipo tafiti za wataalamu mbalimbali, zikionesha kuwa asilimia kubwa ya paka weusi ni wa jinsia ya kiume.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img