2.8 C
New York

Miaka miwili ya vita: Israel imefanikiwa nini Gaza?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
NI miaka miwili sasa tangu wapiganaji wa Hamas walipoishambulia Israel. Shambulizi hilo la Oktoba 7, mwaka 2023 liligharimu maisha ya watu 12,000 na wengine 251 walishikiliwa mateka.
Tangu Hamas ilipofanya shambulizi hilo lililotikisa siasa za Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla, Israel haijaacha kufanya mashambulizi mazito kwa Wapalestina waishio Ukanda wa Gaza.
Operesheni mbalimbali za jeshi la Israel (IDF) zimeshuhudia vifo vya watu takribani 66,000, ambapo asilimia 80 wanatajwa kuwa ni raia wasio na hatia.
Kwa mujibu wa Hamas, majeruhi ni zaidi ya 169,000, wakati huo pia jumuhiya za kimataifa zikieleza kuwa idadi ya vifo vya raia wasio na hatia ni kubwa kuliko inavyoripotiwa.
Kwa upande wake, Taasisi ya Kimataifa ya Wahamiaji inaeleza kuwa mashambulizi ya Israel yamesababisha watu milioni 1.9 kukosa makazi huko Gaza.
Mbaya zaidi, hatua ya Israel kuzuia misaada kuingia Gaza imeripotiwa mara kadhaa kusababisha vifo 450 vitokanavyo na njaa. Kati ya 450, vifo 150 ni vya watoto.
Je, ikiwa ni miaka miwili sasa ya vita, Israel imefanikiwa katika kile ilichokusudia katika Ukanda wa Gaza baada ya kumshambuliwa na Hamas mwaka 2003? Makala haya yanachambua.
Baada ya shambulizi la Oktoba 7, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema wana malengo makubwa mawili katika vita ya Gaza. Mosi, ni kurejesha mateka waliochukuliwa na Hamas. Pili, ni kuliangamiza Kundi hilo.
Hata hivyo, hakuna alichofanikiwa kufikia sasa. Kati ya mateka 251, ni 148 pekee waliorejea Israel wakiwa hai. Serikali ya Israel inakiri kati ya mateka 48 wanaoshikiliwa na Hamas, huenda ni 20 pekee wanaoweza kuwa hai.
Kuhusu kuiangamiza Hamas, bado Israel haijafanikiwa kwa asilimia 100. Licha ya wanajeshi wa Israel kuwaua wapiganaji wengi wa Hamas, bado hawajafanikiwa kulitokomeza Kundi hilo.
Nguvu kubwa ya Hamas inatokana na ushirikiano wake na makundi mawili ya Hezbollah, ambalo lina makazi yake Lebanon, na Houthis la Yemen. Kwa pamoja, makundi hayo yanatajwa kuwezeshwa kiuchumi na Serikali ya Iran.
Licha ya kumuua kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, kuishambulia Iran na kumuua kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, bado Israel haijaweza kumaliza ushindani mkali inaoupata kutoka kwa vikundi hivyo.
Mbali ya hilo, Israel imekuwa ikitupiwa lawama na jumuhiya za kimataifa kwa namna inavyofanya mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza.
Kwamba badala ya kuwalenga wale inaowaita magaidi, imekuwa ikishambulia maeneo ya hospitali, kambi za wakimbikizi na shule, hivyo kusababisha mauaji ya watoto, wanawake, waandishi wa habari na wafanyakazi wa mashirika ya misaada.
Ni kutokana na mazingira hayo, jumuhiya za kimataifa, ukiwamo Umoja wa Mataifa kupitia Tume yake ya Haki Binadamu, zinailaani Israel zikiitaja kujihusisha na mauaji ya halaiki.
Desemba, 2023, Afrika Kusini ilipaza sauti na kuishitaki Israel kwa madai ya kutekeleza mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza. Pia, mwaka jana, Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) nayo iliagiza Netanyahu na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant, wakamatwe kwa tuhuma hizo.
Baadaye, Serikali ya Israel na washirika wake waliipinga hati ya kukamatwa kwa viongozi hao. Kwa kuiunga mkono Israel, hatimaye Hungary ilitangaza kujitoa ICC.
Wakati huo huo, pigo jingine kwa Israel ni namna Palestina inavyovuna ushawishi mbele ya mataifa mengine tangu vita ilipoanza Oktoba 7.
Kabla ya vita, takribani mataifa 140 yalikuwa yakiiunga mkono Palestina katika harakati zake za kutambulika kama nchi huru. Tangu Oktoba 7, yameongezeka mataifa mengine 20 kuiunga mkono. Miongoni mwao ni Ufaransa, Uingereza, Hispania, Australia na Canada.
Pia, ukiweka kando kuchagua upande wa Palestina, baadhi ya mataifa yaamenda mbali zaidi na kuiwekea vikwazo Israel. Mataifa hayo ni pamoja na Colombia, Afrika Kusini na Malaysia.
Vilevile, Israel haiungwi mkono na raia wake wanaotaka kuona Serikali yao ikiliagiza jeshi kuacha mara moja mashambulizi inayofanya katika Ukanda wa Gaza. Utafiti wa Julai, mwaka huu, unaeleza kuwa asilimia 60 ya wanachi hawakubaliani na vita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img