2.8 C
New York

Zelensky aonya Urusi kuvamia mataifa mengine

Published:

KYIV, Ukraine
URUSI itaendelea kuvamia mataifa mengine ya Ulaya endapo Umoja wa Mataifa hautachukua hatua za kuizuia.
Aliyesema hayo ni Rais wa Ukraine, Zelensky, wakati alipokuwa akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo mjini New York, Marekani.
Zelensky, ambaye Taifa lake limevamiwa kijeshi na Urusi, ameonya kuwa Rais Vladimir Putin hataishia hapo, bali atataka kuteka maeneo mengine duniani.
Kauli ya Zelensky imetanguliwa na ile ya Rais wa Marekani, Donald Trump, aliyeahidi kuwa Ukraine itarejesha ardhi yake iliyoporwa na Urusi.
Hata hivyo, Zelensky amekosoa pia jumuhiya za kimataifa akiita kuwa ni dhaifu na zisizo na nguvu ya kuitetea Ukraine dhidi ya uonevu wa Urusi.
Ametolea mfano mataifa ya Georgia na Belarus, akisema Umoja wa Ulaya umeshindwa kuzisaidia nchi hizo wakati huu zikiwa chini ya utawala wa Urusi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img