7.6 C
New York

Mutharika arudi Ikulu, Chakwera akubali yaishe

Published:

LILONGWE, Malawi
ALIYEWAHI kuwa Rais wa Malawi, Peter Mutharika, ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika wiki iliyopita.
Wakati huo huo, aliyekuwa mpinzani wake mkubwa, Lazarus Chakwera, amekubali matokeo, akimpisha Mutharika aliyerudi Ikulu akiwa na umri wa miaka 85.
Katika Uchaguzi huo, Mutharika amepata ushindi wa kishindo baada ya kukusanya asilimia 57 dhidi ya asilimia 33 za Chakwera mwenye umri wa miaka 70.
Chakwera alikiri kushindwa katika matokeo hayo, akienda mbali zaidi na kumpongeza mpinzani wake huo kwa kile alichokiita kuwa ni ushindi wa kihistoria.
Mutharika aliyewahi kuwa profesa wa sheria, alikuwa rais wa Malawi kuanzia mwaka 2014, kabla ya kumpisha Chakwera mwaka 2020.
Kwa upande mwingine, safari hii anaikuta Malawi ikiwa na changamoto kadhaa za kiuchumi, kubwa ikiwa ni mfumuko wa bei unaofikia asilimia 30.
Mutharika ni mdogo wa aliyekuwa Rais wa Malawi, Bingu, ambaye hata hivyo alifariki akiwa madarakani mwaka 2012.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img