BANGKOK, Thailand
MACHAFUKO yanayoendelea katika mpaka wake na Cambodia yameanza kulipa nafasi kubwa jeshi la Thailand kuipindua Serikali iliyoko madarakani katika Taifa hilo la barani Asia.
Thiiland imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi mara 12 tangu mwaka 1931 na huenda uongozi wa sasa wa Serikali ya kiraia nao ukaonja machungu hayo.
Ikumbukwe, Serikali iliyoko madarakani, ambayo si ya kijeshi, iliingia madarakani kwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2023 baada ya jeshi kushikilia nchi tangu mwaka 2014.
Lakini sasa, wakati huu Thailand ikiwa kwenye vita ya mpakani na majirani zao, Cambondia, jeshi lineripotiwa kuanza kujipanga kuichukua nchi kwa mara nyingine.
Kwa wachambuzi, uwepo wa vita hivyo umelipa jeshi uhuru mkubwa wa kujitawala, huku Serikali ikibaki kuwa mtazamaji tu wa kile wa kile kinachoendelea.
Nini chanzo cha mgogoro? Baada ya mwaka mmoja wa uhusiano mbaya kati ya Thailand na Cambodia, mambo yaliharibika zaidi Aprili, mwaka huu. Ni baada ya mwanajeshi wa Cambodia kuuawa na vikosi vya Thailand katika maeneo ya mpakani.
Julai 24, baada ya mapambano ya siku tano kati ya mataifa hayo, watu zaidi ya 40 walioripotiwa kufariki na wengine wengi kujeruhiwa.
Ni kwa kiasi gani jeshi lina nguvu, kiasi cha kutishia uwezekano wa kuipindua Serikali? Katika maeneo ya mikoa ya mpakani ya Thailand, jeshi limeonekana kuwa na nguvu kubwa ya kiutawala, yakiwamo masuala nyeti ya sera ya mipaka.
Kwamba sasa jeshi halihitaji kusubiri maelekezo kutoka serikalini. Ni kama Jenerali Boonsin aliposema Thailand ingeishambulia Cambodia hata bila kusubiri ‘maelekezo kutoka juu’.
Je, wananchi wanazungumziaje juu ya utawala wa kijeshi? Utafiti wa Taasisi moja ya Thailand umebaini kuwa wananchi wanauamini zaidi utawala wa kijeshi katika kulinda na kusimamia masilahi ya Taifa lao na kumaliza mgogoro wao na Cambodia.
Katika utafiti huo, ni asilimia 15 pekee ya wananchi waliosema wana imani na Serikali katika kukabiliana na mambo mawili hayo.
Published:


