MIAMI, Marekani
WENYEJI wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu, Canada, ambao wanashirikiana na Mexico na Marekani, watakwana na Morocco katika hatua inayofuata ya 16 Bora.
Canada chini ya ocha Jesse Marsch, walivuka hatua iliyopita (32 Bora) kwa kuitoa timu nyingine ya Afrika, Afrika Kusini.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Stephen Eustaquio na huo ukawa mwisho wa safari ya Bafana Bafana.
Kwa upande wao, Morocco wametia mguu hatua ya 16 Bora baada ya kuitandika Uholanzi kwa penalti 3-2.
Mchezo huo ulilazimika kuhamia katika changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Uholanzi walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa staa wa Liverpool, Cody Gakpo, lakini Issa Diop aliisawazishia Morocco katika dakika za jioni.
Kwa upande wa Uholanzi, waliokosa penalti zao ni Quentin Timber, Crysencio Summerville na Justin Kluivert.
Mchezo wa hatua ya 16 Bora kati ya Canada na Morocco unatarajiwa kuchezwa Julai 4, 2026.


