31.1 C
New York

Mtibwa yaelekea maisha mapya Championship

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

WAKONGWE wa soka la Morogoro, Mtibwa Sugar, wameiaga rasmi michuano ya Ligi Kuu Bara, hivyo msimu ujao watacheza Ligi Daraja la Kwanza (Championship).

Safari yao kwenye Ligi imehitimishwa leo Juni 30, 2026 kwa kichapo cha mabao 2-1 ugenini dhidi ya Namungo.

Baada ya michezo 30, Mtibwa Sugar imeondoka Ligi Kuu ikiwa imeshinda sita, sare tisa na kufungwa mara 15, hivyo kujikusanyia pointi 27.

Ni kwa maana hiyo, imemaliza msimu huu wa 2025-26 ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi.

Kwamba sasa imeungana rasmi na KMC ambayo ilishashuka Daraja ikiwa mkiani kwa pointi tisa pekee katika michezo 30.

Related articles

Recent articles