33.6 C
New York

Mshukiwa mauaji ya Rwanda akamatwa Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani

WAENDESHA mashitaka wa Ujerumani wamethibitisha kukamatwa kwa mwanaume anayehusishwa na mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.

Mwaka huo, Rwanda iliingia kwenye machafuko ya siku 100 mfululizo yaliyoshuhudia makabila makubwa mawili; Tutsi na Hutu.

Katika machafuko hayo, Watutsi wanaotajwa kuwa ni zaidi ya 800,000 na Wahutu kadhaa walipoteza maisha.

Mwanaume aliyekamatwa katika Jimbo la Hesse, Ujerumani anayefahamika kama Innocent S, anatajwa kutoa amri kwa watu wake kuuawa Watutsi 25.

Kwa mujibu wa waendesha mashitaka, wakati huo alikuwa msaidizi wa Meya wa Jimbo la Kayove, Kaskazini-Magharibi mwa Rwanda.

Related articles

Recent articles