31.4 C
New York

Kocha Ujerumani agoma kujiuzulu

Published:

MUNICH, Ujerumani

BAADA ya timu ya soka ya Taifa ya Ujerumani kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia, kocha wake, Julian Nagelsmann, amesema hana mpango wa kujiuzulu.

Ujerumani iliondoshwa na Paraguay kwa penalti 4-3, mchezo ambao dakika 120 zilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kwa upande wake, Nagelsmann amedai kuwa hajafikiria kujiuzulu, hivyo atalazimika kufanya hivyo endapo tu Shirikisho la Soka la Ujerumani litaamua.

Ifahamike kuwa mkataba wake wa kuliongoza benchi la ufundi la Ujerumani bado unaendelea, ukitarajiwa kufikia ukomo mwaka 2028.

“Bado nipo. Kama wanataka nibaki hadi 2028, nitafanya hivyo. Na kama hawanitaki, nitaondoka,” amesema Nagelsmann.

Related articles

Recent articles