31.4 C
New York

Kama ulivyosikia! Yanga wabeba tena ‘ndoo’ Ligi Kuu

Published:

Na Hassan Mwasha

HATIMAYE Yanga wamethibitisha ubabe wao Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza msimu huu wa 2025-26 kwa kutwaa ubingwa wao wa tano mfululizo.

Yanga wamenyakua taji hilo leo Juni 30, 2026, kwa kuitandika JKT Tanzania mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa msimu.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, ‘Timu ya Wananchi’ ikiwa ugenini ilipata mabao yake kupitia kwa Prince Dube, Maxi Nzengeli, na Depu.

Safari hii, Yanga wamebeba ‘ndoo’ baada ya kufikisha pointi 75, ikiizidi mbili Simba iliyomaliza nafasi ya pili kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC.

Kwa upande mwingine, Wanajangwani hao wamefikisha mabao 71, huku nyavu zao zikiwa zimetikiswa mara tisa pekee katika michezo 30.

Wakati huo huo, Yanga wamefunga msimu huu kibabe kwani wameshinda mechi 23, wamepoteza moja (3-2 dhidi ya Dodoma Jiji), na kupata sare sita.

Taji hilo la Ligi Kuu Bara halijaondoka Mitaa ya Twiga na Jangwani tangu lilipotua msimu wa 2021-22, ambapo walimaliza bila kufungwa (unbeaten).

Related articles

Recent articles