RIO, Brazil
LICHA ya timu ya soka ya Taifa ya Brazil kutinga hatua ya 16 Bora ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026), kocha Carlo Ancelotti amepewa onyo kali.
Brazil, maarufu kwa jina la ‘Selecao’ (Wateule), imevuka hatua ya 32 Bora baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Japan.
Katika mtanange huo, Brazil ilipata mabao yake kupitia kwa mkongwe Casemiro na staa wa Arsenal, Gabriel Martinelli.
Hata hivyo, mkongwe wa klabu ya Corinthians ya Brazil, Craque Neto, amesema kiwango cha timu hiyo dhidi ya Japan hakitoi picha nzuri kuelekea hatua ya 16 Bora.
Aidha, Neto ameeleza kushangazwa na uamuzi wa kocha Ancelotti kutokumchezesha Neymar katika mechi hiyo dhidi ya Japan.
“Dhidi ya Japan humchezeshi Neymar? Mpe nafasi. Unataka acheze robo fainali? Nusu fainali? Fainali? Huo ni utani,” amesema Neto, ambaye alistaafu akiwa ameitumikia Brazil katika mechi 15 kati ya mwaka 1988 na 1993.


