10.7 C
New York

Utafiti: Matumizi ya feni chanzo ugonjwa wa moyo

Published:

LOS ANGELES, Marekani
LICHA ya umuhimu wake, hasa kwa maeneo yenye hali ya hewa ya joto, matumizi ya feni yanaweza kuwa na madhara kwa afya yako, kwa mujibu wa utafiti mpya.
Utafiti huo wa Chuo Kikuu cha Sydney nchini Australia umebaini kuwa watumiaji wa feni wakati wa joto kali wako hatarini kupata ugonjwa wa shambulio la moyo.
Katika utafiti wao, wataalamu hao walitumia ‘sampo’ ya watu 20 kuchunguza athari za kiafya zinazoweza kujitokeza pindi feni inapotumika wakati wa joto kali.
Majibu ya utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Emergency Medicine yalionesha kuwa watu waliokuwa kwenye joto kali, kisha wakawasha feni, walikuwa hatarini zaidi.
Akifafanua zaidi, mtaalamu aliyeongoza utafiti huo, Dkt. Connor Graham, alisema hali ya joto inayoweza kuwa rafiki kwa matumizi ya feni hapaswi kuzidi nyuzi 39. “Ikiwa joto ni zaidi ya nyuzi 40, ni bora kuzima feni tu,” anasema Dkt. Graham.
Lakini pia, watafiti hao wanashauri kuwa kwa watu wenye umri chini ya miaka 40, ni vizuri zaidi kutumia feni endapo hali ya hewa ni joto chini ya nyuzi 39.
Ni tofauti ya watu wenye umri wa miaka 65 au zaidi ambao wanashauriwa kutumia feni katika mazingira ya joto yenye kiwango cha chini ya nyuzi 38.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img