7.8 C
New York

Utafiti: Mboga za majani kinga dhidi ya saratani

Published:

LOS ANGELES, Marekani
KUEPUKA ulaji wa nyama na badala yake kutumia mboga za majani kutakuepusha na ugonjwa wa saratani kwa asilimia 25, utafiti unaeleza.
Tafiti nyingi za hivi karibuni zimeonesha kuwa kumekuwapo na ongezeko kubwa (27%) la vijana wanaosumbuliwa na ugonjwa wa saratani.
Hali ni mbaya zaidi kwa Uingereza, ambapo ongezeko la asilimia 3.6 kila mwaka limewashitua wataalamu wa afya wakisema mfumo wa maisha unachangia kwa kiasi kikubwa.
Sasa, utafiti wa wataalamu wa afya nchini Marekani uliohusisha watu takribani 80,000 umebaini kuwa ulaji wa mboga za majani hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti kwa asilimia 12.
Pia, utafiti huo umebaini kuwa walaji wa mara kwa mara wa mboga za majani hujiepusha Kwa asilimia 45 kupata saratani ya tumbo.
Kwa upande mwingine, ulaji wa mayai wametajwa kuwa na uwezekano mkubwa (45%) wa kuepuka saratani ya damu.
Hata hivyo, licha ya mfumo wa maisha, ikiwamo aina ya vyakula, utafiti umetaja sababu za kimazingira nazo kuchangia uwezekano wa kupata saratani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img