12.5 C
New York

Utafiti: Ugumu wa maisha chanzo utoaji mimba Uingereza

Published:

LONDON, England
MATUKIO ya utoaji wa mimba yameripotiwa kuongezeka kwa kasi nchini Uingereza, huku kupanda kwa gharama za maisha kukitajwa kuwa moja ya sababu.
Utoaji wa mimba si kosa nchini Uingereza na inaruhusiwa kupitia Sheria iliyotungwa miaka 60 iliyopita.
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, utoaji wa mimba unaruhusiwa endapo zitakakuwepo sababu za kiafya au pale mwanamke anapohisi hatomudu gharama za kumlea mtoto atakayezaliwa.
Kupitia Sheria hiyo ya mwaka 1967, mwanamke anaweza kuomba kutoa mimba yenye ukubwa wa hadi wiki 24.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Uingereza (ONS), kasi ya utoaji wa mimba imepanda kwa asilimia 29.7, ukilinganisha na asilimia 26.5 kwa mwaka 2021.
Utafiti uliohusisha Visiwa vya England na Wales umebaini kuwa kulikuwa na matukio ya utoaji mimba 247,703 kwa mwaka 2022.
Aidha, ripoti ya utafiti huo inaeleza kuwa wahusika wa matukio hayo ni wale wenye umri kati ya miaka 15 hadi 44.
Wakati huo huo, utafiti unaonesha kuwa wasichana wenye umri chini ya miaka 16 wametajwa kujihusisha zaidi (61%) na utoaji wa mimba.
Ni tofauti na kundi la wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 34, ambao kiwango chao cha utoaji wa mimba ni mmoja kati ya watano.
Lakini, utafiti huo umebaini kuwa wanawake wasioolewa wanaongoza kwa asilimia kubwa katika utoaji wa mimba, tofauti na wenzao walio kwenye ndoa.
Sasa, achilia mbali kupanda kwa gharama za maisha, pia zipo sababu zingine zilizotajwa kuchangia hali hiyo.
Miongoni mwa sababu hizo ni upatikanaji holela wa dawa za kutoa mimba. Kwamba kundi la vijana limekuwa likizipata kwa urahisi na kuzitumia wakiwa nyumbani.
Kwa upande mwingine, utafiti uliitaja Liverpool na Brighton kuwa ndiyo miji inayoongoza kwa matukio ya utoaji wa mimba nchini Uingereza.
Katika miji hiyo mikongwe, asilimia zaidi ya 40 ya mimba ziliishia kutolewa katika mazingira tofauti.
Pia, miji ya London na Cheshire nayo ilitajwa kuwa na matukio mengi ya aina hiyo kwa kiwango cha asilimia 38.4 na 38.1.
Ni tofauti na Cambridgeshire, mji ambao unatajwa kuwa na kiwango kidogo zaidi (18.6%) cha matukio ya utoaji wa mimba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img