13.9 C
New York

Pioli atimka Saudia, arudi Italia

Published:

ROMA, Italia

BAADA ya msimu mmoja wa kuinoa Al-Nassr, kocha raia wa Italia, Stefano Pioli, ameondoka klabuni hapo.
Pioli mwenye umri wa miaka 59, amerejea nyumbani, Italia, na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Fiorentina kwa mkataba wa miaka mitatu.

Aliwahi kucheza Fiorentina kuanzia mwaka 1989 hadi 1995, kabla ya kuinoa kwa miaka miwili (2017 – 2019).
Kocha huyo amekwenda kuchukua nafasi ya Raffaele Palladino, ambaye alijiuzulu Juni, mwaka huu, wiki chache baada ya kusaini mkataba utakaokwisha mwaka 2027.

“Fiorentina inatangaza kuwa kocha wake ni Stefano Pioli,” ilieleza taarifa ya Fiorentina.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img